Thursday, September 8, 2016

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

Azam FC, jana jioni imeandika rekodi mpya kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya baada ya kuichapa kwa mara ya kwanza  Tanzania Prisons ndani ya uwanja huo kufuatia ushindi wa bao 1-0 ilioupata katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Kwa miaka mingi sasa tokea Azam FC ipande Ligi Kuu Julai 27, 2008, ilikuwa haijawahi kuwafunga maafande hao ndani ya uwanja huo, ambapo mara nyingi imekuwa ikiambulia sare na kupoteza lakini leo imeweza kutakata vilivyo ikiwa chini ya makocha kutoka Hispania wakiongozwa na Kocha Mkuu, Zeben Hernandez.
Ushindi huo umeifanya Azam FC kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa inalingana kwa kila kitu na Mbeya City (GD 4) inayoshika nafasi ya pili wote wakiwa na pointi saba, sawa na Simba inayokamata nafasi ya tatu, lakini wao wanazidiwa tofauti ya mabao kufunga na kufungwa (GD 3).
Shujaa wa Azam FC kwenye mchezo huo ni kiungo mkabaji Michael Bolou, ambaye amefunga bao hilo pekee dakika ya 59 akiunganisha pasi safi ya beki Shomari Kapombe, ambapo mfungaji alipiga shuti kali akiwa ndani ya eneo la 18 na mpira kugonga mwamba wa juu na kujaa wavuni.
Azam FC licha ya kupata ushindi huo, imekutana na upinzani mkali kutoka kwa wapinzani wao, ambao kwa mara kadhaa mashambulizi yao yalikuwa yakiishia kwa mabeki na kipa Aishi Manula, aliyeendeleza ubora wake baada ya kufanya kazi kubwa ya kuokoa michomo kadhaa ya wachezaji wa maafande hao.
Kwa mara ya kwanza leo, ilishuhudiwa beki mpya wa Azam FC, Daniel Amoah, akicheza mechi yake ya kwanza tokea ajiunge na timu hiyo msimu huu akitokea Medeama ya Ghana, ambapo ameonekana kufanya vizuri kwa nafasi mbili alizochezeshwa kipindi cha kwanza akianzia upande wa kulia kabla ya kucheza ‘sentahafu’ kipindi cha pili. Pia mshambuliaji Gonazo Bi Thomas kutoka Ivory Coast, naye alicheza mechi ya kwanza
Mchezo huo ulishuhudiwa ukimalizika kwa sare ya bila kufungana kipindi cha kwanza, ambapo mpira ulibadilika kipindi cha pili kwa wachezaji wa Azam FC kulishambulia sana lango la Prisons hadi kupata bao hilo la ushindi.
Mara baada ya bao kuingia, mpira ulibadilika tena ambapo kila timu ilionekana kucheza mipira mingi mirefu hadi mwishoni mwa mchezo huo.
Nahodha wa Azam FC, John Bocco, aliye kileleni kwenye ufungaji bora akiwa na mabao matatu, alikaribia kuandika bao la pili kwa upande wa timu hiyo lakini shuti alilopiga wakati akizongwa na mabeki wa Prisons lilipaa juu ya lango.
Mara baada ya mchezo huo, Azam FC itakamilisha mechi yake ya mwisho jijini hapa Mbeya msimu huu kwa kucheza na Mbeya City Jumamosi ijayo (Septemba 10).
Zeben na rekodi mbili
Wakati leo akivunja mwiko wa Azam FC kutopata ushindi dhidi ya maafande hao jijini hapa, Zeben hivi sasa ameshavunja rekodi nyingine ya timu hiyo kutochukua taji la Ngao ya Jamii katika fainali tatu tofauti.
Hii ni baada ya kuingoza Azam FC kutwaa taji hilo mwanzoni mwa msimu huu kwa kuichapa Yanga kwa mikwaju ya penalti 4-1 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
Kikosi Kilivyokuwa:
Aishi Manula, Shomari Kapombe, Bruce Kangwa/Khamis Mcha dk 84, Daniel Amoah, David Mwantika, Jean Mugiraneza, Himid Mao, Michael Bolou/Frank Domayo dk 80, Salum Abubakar, John Bocco (c), Gonazo Bi Thomas/Shaban Idd dk 73

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video