Thursday, September 1, 2016

MAAFANDE wa  JKT Ruvu Stars  baada kuahirishwa kwa mchezo wao dhidi ya Mabingwa Watetezi Yanga SC uliotakiwa kuchezwa Jana uwanja wa Taifa, Dar es salaam, hivi sasa wameelekeza nguvu zao kwenye mechi ya mwishoni mwa Juma hili ambapo wataikabili African Lyon  Uwanja wa Mabatani, Mlandizi, Pwani.
Msemaji wa JKT Ruvu, Afisa Mteule Daraja la Pili, Constantine Masanja amesema: “Hivi sasa timu inaendelea na mazoezi katika kambi ya JKT Mbweni chini ya kocha mkuu Comred Denis Malale Hamsini”.


Aidha, Masanja ameeleza kuwa wachezaji wanne waliokuwa kwenye Mashindano ya Majeshi kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyomalizika mwezi uliopita Kigali, Rwanda, watajiunga na kambi wakati wowote.

Wachezaji hao ni Paul Mhadize, Hamis Seif, Emmanuel Pius na Juma Mussa Kiumbu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video