Saturday, September 17, 2016

Alexis Sanchez amefunga mara mbili na kukosa penati na kuiongoza Arsenal kushinda mabao 4-1 dhidi ya Hull City pungufu kwenye mchezo wa Premier League uliopigwa KCOM Stadium.

Sanchez aliipa Arsenal goli la kwanza kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Alex Iwobi, lakini alishindwa kufunga bao la pili baada ya kukosa mkwaju wa penati uliosababishwa na Jake Livermore kabla ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Theo Walcott alifunga bao la pili dakika ya 55 kabla ya Robert Snodgrass kufunga bao pekee kwa Hull City kwenye mchezo huo kwa mkwaju wa penati.

Sanchez alifunga bao la tatu dakika ya 83 kabla ya Granit Xhaka kumaliza karamu ya magoli dakika ya 90 kwa Arsenal kwa kufunga bao la nne kwa shuti kali.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video