Thursday, July 28, 2016

Kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi mchezaji mpya wa Liverpool Ragnar Klaven katika mchezo wa michuano ya International Champions Cup (ICC), inayoendelea nchini Marekani kwa lengo la kuziandaa baadhi ya klabu za barani Ulaya, kwa ajili ya msimu wa 2016/07 ambao utaanza rasmi mwezi ujao.
Fabregas, 29, alifanya faulo hiyo kwa kuinua kiatu chake juu ya mguu wa mchezaji huyo wa Liverpool, na ndipo mwamuzi alioamua kuchukua maamuzi hayo.
Katika mchezo huo, Chelsea wameibuka wababe kwa kushinda bao 1-0, lililofungwa na beki Gary Cahill baada ya dakika 10 tu za mchezo kufuatia kuunganisha mpira wa kona uliochongwa na Cesc Fabregas.
Bosi wa Liverpool Jurgen Klopp amethibitisha kwamba baada ya mchezo Fabregas alienda kwenye chumba cha kubadilishia mavazi cha Liverpool ili kuomba radhi kwa tukio hilo.
Kwa upande wake bosi wa Chelsea, Antonio Conte vile vile ameomba radhi kwa kitendo hicho na kusisitiza kwamba halikuwa tukio la kukusudiwa.
"Nadhani uchovu wakati mwingine unaweza kusababisha mchezaji kuchelewa kufanya maamuzi kwenye tukio la uwanjani," amesema.
"Nafahamu kwamba Fabregas ni mtu mzuri sana, kijana mzuri na sio aina ya wachezaji ambao wana tabia kama hizi. Namwombea msamaha kwenu, pia nampa pole mchezaji wa Liverpool."

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video