Simba SC imeanza vyema maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa ligi baada ya kuichapa Polisi Moro mabao 6-0, mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Wakicheza kwa umahiri mkubwa chini ya kocha wao mpya Mcameroon Joseph Omog, Simba walionekana kuimarika hasa safu yao ya ushambuliaji iliyokuwa chini ya Ibrahim Ajib .
Magoli ya Simba yalifungwa na mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Frederick Blagnon (2) dakika ya 5 na 16, sawa na Ibrahim Ajib dakika 48 na 73, huku mengine yakiwekwa kimiani na Mohammed Mussa dakika ya 82 na Abdi Banda dakika ya 85.
Simba ambayo kwa sasa imejikita mkoani Morogoro kwenye Chuo cha Biblia kwa ajili ya kambi kujiandaa na msimu mpya, inaonekana kuimarika siku hadi siku huku ikitegemea kufanya mambo makubwa pale msimu mpya wa ligi utakapofunguliwa.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Janvier Besala Bokungu/Hamad Juma dk46, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’/Abdi Banda dk59, Method Mwanjali, Novat Lufunga/Juuko Murushid dk46, Muzamil Yassin, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Said Ndemla dk46, Shizza Kichuya/Mohammed Mussa dk70, Frederick Blagnon/Mussa Mgosi dk25/Peter Mwalyanzi dk70, Ibrahim Hajib/Awadh Juma dk75 na Jamal Mnyate/Danny Lyanga dk46.
0 comments:
Post a Comment