Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta anatarajiwa kuingia dimbani hii leo wakati klabu yake ya Genk ikimenyana na Cork City FC ya Ireland katika raundi ya tatu ya ya mchujo wa kufuzu hatua ya makundi ya Europa League.
Wenyeji Genk wanapigwa upatu kushinda pambano la leo na kujiweka mazingira mazuri ya mechi ya marudiano itakayochezwa Agosti 4 huko Ireland.
Mshindi wa jumla wa pambano la leo na lile la marudiano atafuzu kwa hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi, ambako Manchester United tayari inawsubiria.
Pambano litapigwa majira ya saa tatu usiku. Samatta ameanza vizuri katika mechi za Europa akiwa tayari amefunga bao moja, amepika bao moja pamoja na kufunga penati kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Buducnost iliyoamuliwa kwa mikwaju ya penati baada ya sare ya jumla ya mabao 2-2.
0 comments:
Post a Comment