Je, Paul Pogba anaenda Manchester United? Kiungo huyo anafanya kila liwezekanalo kumfikirisha kila mtu abaki njia panda kama anaondoka ama la.
United wameshafikia makubaliano ya awali ya kumsajili kiungo huyo wa Juventus kwa ada ya itakayovunja rekodi ya euro mil 110.
Juventus wamekuwa wakikanusha uvumi wa nyota huyo kuondoka msimu huu, huku pia wakala wake Mino Raiola akikaa kuthibitisha kama uhamisho umekamilika ama la.
Na sasa Pogba, ambaye kwa sasa yupo mapumzikoni baada ya Michuano ya Euro kumalizika ameposti picha kwenye akaunti yake ya Instagram yenye maelezo: “we say it all by saying nothing at all #holidays.”
0 comments:
Post a Comment