Friday, July 29, 2016

Bilionea kijana zaidi wa Kitanzania na Mfanyabiashara mkubwa nchini na Afrika kwa ujumla Mohammed Dewji 'MO' amesema, dhumuni na ahadi yake ya kuifanya Simba iwe ya kisasa endapo klabu hiyo itakubali mfumo wa hisa liko pale pale.

Dewji ambaye ni hapo awali alishawahi kuidhamini Simba amesema kwamba kwa sasa Simba huwezi kulinnganisha na Yanga wala Azama na ikichukuliwa kwa uzani, basi bejeti ya Yanga na ile ya Azam ni mara mbia habari katika mkutano uliofanyika leo jijini DAr es Salaam kwamba bajeti ya Yanga na Azam FC ni mara mbili ya ile ya Simba ya sasa, jambo linaloifanya klabu hiyo kuendelea kubaki kuwa msindikizaji kwenye ligi na michuano mingine hapa nchini.

Katika mkutano wake na wabahabari uliofanyika jijini Dar es Salaam, MO amesma kwamba yuko tayari kuanzia sasa kutoa Sh bilioni 20 ili kununua asilimia 51 ya hisa zote na kuwekeza ndani ya Simba, uwekezaji ambao utakuwa na ambao mengi ndani yake.

“Kama unataka mafanikio kwenye mpira, hakuna zaidi ya fedha. Simba haiwezi kuwa na miaka 80 leo haina hata uwanja wa mazoezi.

"Uwekezaji huu utajumuisha kujenga uwanja wa mazoezi, kuandaa timu za vijana, mishahara minono ya wachezaji bila kusahau swimming pool, vitu ambavyo ni muhimu sana kwa wachezaji wa kisasa," alisema.

“Unajua kama nikiwekeza fedha hizo, tunaweza kuzipeleka kwenye mkopo na kuikopesha serikali. Baada ya hapo tutapata faida ya dola bilioni 7.5 ambazo tutaziingiza kwenye maendeleo.

“Mimi ninaamini Simba haiwezi kubadilika kwa kuwekeza kwenye bajeti ya Sh milioni 500 kwa mwaka. Haitawezekana, ndiyo maana nimekuwa nikisisitiza, kwanza Simba inahitaji muwekezaji na si mdhamini.

“Nisisitize hili,mimi ni mwanachama wa Simba, ninaumia kuona timu hii inakwenda hivi. Ndiyo maana ninaingia nikiamini nitaweza kubadilisha mambo kwa kushirikiana na wanachama wa Simba ili kuleta mabadiliko katika klabu yetu.”

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video