Saturday, March 19, 2016

Inawezaekana isiwe ni taarifa nzuri sana kwa mashabiki wa Yanga, ila ndiyo ukweli ulivyo. Kilichokuwa kikisubiriwa kwa hamu kuwa ni timu gani ambayo Yanga ingekutana nayo baada ya kuwatoa APR ya Rwanda kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika sasa imedhihirika.
Hatimaye sasa Yanga itakabiliana na klabu ya Al-Ahly baada ya vigogo hao wa Misri kuwatupa nje Wababe wa Angola Recreativo Libolo (Clube Recreativo Desportivo do Libolo) baada ya kuwatoa kwa wastani wa 2-0.
Katika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka  suluhu na katika mchezo wa marudiano uliopigwa leo hii nchini Misri Al-Ahly wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, hivyo kusonga mbele katika hatua ya pili ya michuano.
Jioni ya leo katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga imetoka sare ya bao 1-1 na APR ya Rwanda hivyo kuiondoa mashindanoni kwa jumla ya mabao 3-2. Katika mchezo wa awali jijini Kigali vijana hao wa Jangwani waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Yanga haina historia nzuri linapokuja suala la kuziondoa mashindano timu za kiarabu lakini inaonekana mwaka huu wamepania kufika mbali kutokana na usajili kabambe walioufanya.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video