
"Naijua vizuri APR, ni timu iliyonilea kabla sijahamia Yanga SC. Ni timu nzuri sio ya kubeza tunaenda kupambana nao kwa lengo moja tu la kushinda ili kujiweka mazingira mazuri kwa hatua inayofuata na kupunguza presha kwa mchezo wa marudiano.
"Umoja na ushirikiano ni mhimu mashabiki watuunge mkono kama unavyoona tayari tunaungwa mkono na baadhi ya mashabiki mjini hapa. . Mashabiki wetu walioshindwa kuja kutushangilia uwanjani tunaomba wasisahau kutuombea dua"
Ni maneno ya nahodha wa timu ya Taifa ya Rwanda Haruna Niyonzima akizungumzia mchezo wa kesho utakaopigwa katika dimba la Amahoro kuanzia saa 8 mchana kwa saa za Tanzania huku ukirushwa moja kwa moja na Azam Tv.
Credit:Naipenda Yanga facebook page.
0 comments:
Post a Comment