KIUNGO Justice Majabvi wa Simba amemmwagia sifa kiungo Jonas Mkude na kusisitiza kwamba kila siku anazidi kuimarika.
“Mkude yupo vizuri kila siku anabadilka na wote hilo mmeliona katika mechi za karibuni anapambana na nadhani atazidi kuisaidia Simba siku zijazo,”aliiambia Mwanaspoti.
“Kwangu mimi namuona ni kijana mdogo, huwa anajifunza vingi kwangu na nimekuwa nikimulekeza, anaelewa na anafanyia kazi ushauri wangu,”alisema .
Majabvi alisema kinachowafanya wacheze vizuri ni maelewano na kufuata maelekezo ya kocha na ndio maana wamezidi kuimarika siku hadi siku.
Katika safu ya kiungo Simba imeonekana kuimarika siku hadi siku na viungo wa timu pinzani wamekuwa wakipata wakati mgumu wakikutana nao.

0 comments:
Post a Comment