
Chelsea wameshatoka kwenye Champions League msimu huu na uhakina msimu ujao pia wameshatoka, lakini Hazard ndio amekua headline kwa upande wa Chelsea zaidi ya kufungwa kwa timu yake.
Kama ulifuatilia mchezo vizuri utakua uliona kipindi cha kwanza kilivyoisha Eden Hazard alibadilishana jezi na Angel di Maria ambapo sio utaratibu wa kawaida. Pia wakati ule kila mchezaji anatakiwa ku-focus kwenye mchezo zaidi ya kitu kingine chochote.
Baada ya kufanya vile baadaye mashabiki walimzomea mchezaji huyo ambae kwa muda mrefu analalamikiwa kwak kucheza chini ya kiwango ikisemekana anashinikiza kutaka kuhama club ya Chelsea.
Hiddink alisema,“Mashabiki wa Chelsea walikuwa na haki na ni sawa walivyomzomea Hazard, wana haki ya kuonyesha kutopendezwa na kitu chochote ambacho wanadhani sio sahihi”. Baadae Roy Keane kwenye kituo cha ITV pia alimponda Hazard kwa kitendo hicho hicho.
Roy Kean alisema,“Ninaogopa hata kuzungumzia hili swala, mchezaji akiwa kwenye mechi kubwa akili yake yote inatakiwa kuwa kwenye mchezo na sio kitu kingine. Mimi hata mwisho wa mchezo nisingepoteza muda wa kubadirishana jezi, sasa mtu anafanyaje hivyo muda wa half time”.

0 comments:
Post a Comment