Wednesday, March 2, 2016

Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi Tanzania (Frat), Mwalimu Nassor, amesema kitendo cha timu ya Azam kugomea kuchezeshwa na mwamuzi, Emmanuel Mwandembwa kwao hakijawashtua sana kwani matukio kama hayo ya kukataliwa kwa waamuzi wao, wameshayazoea.
Juzi Jumatatu kabla ya mchezo wa Kombe la FA kati ya Azam na Panone FC uliopigwa kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi, Azam ilikataa kuchezeshwa na Mwandembwa kwa madai kuwa aliwanyonga siku chache nyuma walipocheza dhidi ya Coastal Union na kufungwa bao 1-0 katika Ligi Kuu Bara.
Baada ya Azam kumgomea mwamuzi huyo, Chama cha Soka Mkoa wa Arusha (KRFA) kililazimika kumbadilisha na kumpa jukumu hilo, Erick Onoka na Azam kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kusonga robo fainali ya michuano hiyo.
“Suala hilo bado halijanifikia ofisini kwangu lakini hata hivyo matukio ya kukataliwa kwa waamuzi wetu hayajaanza kutokea leo, kama utakumbuka Simba nayo ilimkataa Jonesia Rukyaa asichezeshe mechi yao ya hivi karibuni dhidi ya Yanga, lakini tuliweka misimamo yetu na akachezesha.
“Lakini nadhani hao waliohusika kumbadilisha huyo mwamuzi watakuwa wanawalea Azam kwa sababu wangekomalia sidhani kama wangeendelea kukataa,” alisema Nassor.
Naye Ofisa Habari wa Azam, Jafari Idd, alisema walilazimika kufanya hivyo kutokana na kutokuwana amani na uchezeshaji wa mwamuzi huyo ukizingatia kwamba anatokea mkoani humo.
“Mwamuzi yule alipotuchezesha dhidi ya Coastal kwa mtu aliyeshuhudia mchezo ule nadhani aliona ni jinsi gani hakuwa ‘fair’ kwa upande wetu, halafu katika mechi yetu hii ndiyo atuchezeshe huku tukifahamu kwamba ni mkazi wa Kilimanjaro! Hapo lazima tupate mshtuko,” alisema Idd.
SOURCE: CHAMPIONI

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video