
Boss wa Arsenal anapata support kutoka kwa watu wenye profile kubwa kwenye soka licha ya mashabiki wa Arsenal kutaka kwa hali na mali aachane na club yao.
Baada ya striker wa zamani wa Arsenal Ian Wright kumtetea Wenger licha ya mwenendo mbovu, sasa hivi Beckham ameingia kwenye list ya watu maarufu wanao msupport Wenger. Baada ya kufungwa 2-1 dhidi ya Watford kama kawaida majungu yaliendelea kwenye instagram na social network nyingine.
Kwenye page moja ya mashabiki wa Arsenal ambayo labda Beckham anai follow waliweka post ya picha ya bango ambalo lilikua linasema kwamba kwamba “Arsene Thanks for the memories but it’t time to say good bye.”
Post hiyo kwasababu inafatwa na mashabiki wengi wa Arsenal hivyo basi ilipata comment nyingi za ku support na wengi wakitumia hashtag ya Wenger Out.
Lakini David Beckham aliingia kati kati ya comment nyingi za mashabiki wa Arsenal na kuwachana kwamba hawana shukrani wala heshima na wanatafuta attention.
Maneno hayo yalionyesha moja kwa moja kwamba Beckham licha ya kuwa mchezaji mwenye heshima wa Manchester United lakini bado ana msupport Arsene Wenger kwa kile anachokifanya na Arsenal.


0 comments:
Post a Comment