
Hapo awali iliarifiwa kuwa Lionel Messi angefanyiwa upasuaji ili kuondoa tatizo la figi linalomkabili nyota huyo.
Mshambulizi huyo nyota wa Barcelona alikosa baadhi ya michezo ya Ligi ya Vilabu Bingwa Duniani kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya figo, hivyo klabu yake kuthibitisha kwamba angefanyiwa vipimo jana Jumatatu.
Barca wanatarajia kumwona Messi akirudi mazoezini Jumatano wiki hii, hata hivyo, watu wa karibu na nyota huyo vimethibitisha kuwa suala hilo bado halijafanyiwa maamuzi.
"Taarifa hiz juu ya upasuaji hazina ukweli wowote," chanzo kilisema. "Kikubwa mabacho atafanyiwa ni kuangaliwa mwenendo wa afya yake na kufanyiwa matibabu ya figo ambayo yanamsumbua."
Taarifa hizi ni pigo kubwa kwa mashabiki wa Arsenal baada ya hapo awali kuripotiwa kwamba endapo Messia angefanyiwa upasuaji huo, basi angekaa nje kwa kipindi kirefu na hivyo kuukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Arsenal. lakini kwa mujibu wa taarifa hizi mpya mpya, Mess ataendelea kutoa huduma kama kawaida kunako klabu yake pendwa.
0 comments:
Post a Comment