
Mbwana Samatta amecheza kwa mara ya kwanza kwenye klabu Genk ambayo amejiunga nayo hivi karibuni ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Ubelgiji inayofahamika zaidi kwa jina la Belgium Pro League.
Mchezo huo ulimalizika kwa KRC Genk kupata ushindi wa bao 1-0 ikiwa ugenini kwenye dimba la Stade Le Canounnier. Bao la Genk limefungwa na Thomas Buffel dakika ya 63 akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na winger Nikolaos Karelis.
Mbwana Samatta aliingia dakika ya 73 kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis mtengenezaji wa bao la ushindi.
Ushindi huo unaifanya Genk kufikisha jumla ya pointi 38 ikiwa nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi yenye jumla ya timu 16 baada ya kucheza michezo 25 na kufanikiwa kushinda michezo 11, imepoteza mechi 9 na kutoka sare kwenye michezo 5.
Baada ya mchezo wa huo, Genk itajitupa tena uwanjani Jumamosi ijayo February 13 kuvaana na Waasland-Beveren ambayo ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi hiyo. Mechi hiyo itachezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Genk Cristal Arena.
0 comments:
Post a Comment