
Licha ya kupitia misukosuko mingi kunako klabu ya Chelsea, lakini John Obi Mikel amebaki kuwa mhimili wa klabu hiyo kutokana na sababu mbalimbali.
Kiungo huyo wa Nigeria, amekuwa klabuni hapo na kushuhudia mameneja mbalimbali wakipita klabuni hapo, lakini ujio wa Guus Hiddink umekuwa ni faraja kubwa sana kwake.
Mikel amekuwa akipta nafasi tangu kuwasili kwa Hiddink, na katika kipindi hiki ambacho mashabikimwengi wa Chelsea walipoteza imani na wachezaji wao wengi, lakini Obi amebaki kuwa kati ya wachache wanaoaminiwa sana klabuni hapo.
Hizi ni sababu sita zinazomfanya Obi kuwa legend wa kweli wa Chelsea.
5. Alichagua kujiunga na Chelsea dhidi ya Man United
Kila mtu anafahamu kwa uzuri jinsi ambavyo United walivyokosa Obi wakati wakiwa wamemalizana kila kitu ili kumsajili kutoka klabu ya Lyn ya Norway mwaka 2005, lakini cha ajabu Obi aliamua kujiunga na Chelsea huku akiwa tayari ameshafanya mkutano na wanahabari akiwa na jezi ya Man United.

4. Ana mzigo wa kutosha wa makombe
Licha ya kuwa miaka ya hivi karibuni amekuwa hapati namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza, akiwa Chelsea, Obi amefanikiwa kujinyakulia vikombe vya kutosha na hivyo kabati lake kuwa katika hali maridhawa na kutojutia kukaa klabuni hapo. Amejikusanyia makombe 11 ambayo ni
Premier League (2): 2009–10, 2014–15
FA Cup (4): 2006–07, 2008–09, 2009–10, 2011–12
League Cup (2): 2006–07, 2014-15
FA Community Shield (1): 2009
UEFA Champions League (1): 2011–12
UEFA Europa League (1): 2012–13
Mbali na hayo, Obi amechukua tuzo ya mchezaji bora mwenye umri mdogo zaidi mara mbili.

Na kwa upande wa Afrika, amebeba ndoo ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
3. Si mtu wa kulalamika ovyo
Kwa mara kadhaa, mameneja wa Chelsea wamekuwa wakitimuliwa kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na wachezaji, mfano mzuri ukiwa ni wa Jose Mourinho ambaye alitimuliwa hivi karibuni kwa kesi hiyo, lakini vile vile Andre Villas-Boas. Katika kesi zote hizo, Obi hakuwahi kuhusishwa hata kidogo. Inasemekana na mtu mtulivu na asiye na makuu.

2. Ni moja ya mafundi wasioonekana
Angalia video hii, kisha utathibitisha hili.
1. Ni mwaminifu kwa klabu
Mikel amecheza mara 18 tu msimu uliopita na alikuwa akiingia kutokea benchi kwa takrbani miaka mitatu mfululizo.

Lakini licha ya ugumu wote alioupata katika kipindi chote hicho, Obi hakuwahi kulazimisha kuondoka klabuni hapo japokuwa kulikuwa na ofa kadhaa kutoka klabu za Besiktas na Galatasaray katika kipindi cha dirisha la usajili majira ya joto. Na sasa anafurahia maisha ya kuwa hapo kwa mara nyingine tena.
*Huyu ndiye Jonh Mikel Obi.
0 comments:
Post a Comment