Sunday, February 7, 2016

JKT Ruvu imekubali kichapo cha magoli 4-0 kutoka kwa Yanga na kuirejesha timu hiyo kwenye reli baada ya kuwa na wiki ya tabu kufuatia kupoteza mechi yake ya kwanza kwa goli 1-0 kwenye msimu huu dhidi ya Coastal Union kabla ya kubanwa na kulazimishwa sare ya kufungana bao 2-2 na Tanzania Prisons mkoni Mbeya.
Simon Msuva amefunga magoli mawili kwenye mchezo huku Issoufou Boubacar akifunga goli lake la kwanza kwenye ligi tangu ajiunge na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili na mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe Donald Ngoma aweka goli moja kambani kukamilisha ushindi wa bao nne.
JKT Ruvu wameonekana kucheza vizuri kwenye mchezo wa leo lakini walizidiwa mbinu za kimchezo na Yanga ambao walikuwa wanatumia sana wachezaji wao wa pembeni katika mashambulizi yao mengi.
Ushindi huo unaipa Yanga faida ya kuendelea kubakia kileleni mwa ligi wakiwa wamefikisha jumla ya pointi 43 baada ya kucheza michezo 18 wakifuatiwa na Simba ambao wanapointi 42 wakati nafasi ya tatu ikiwa mikononi mwa Azam ambao leo usiku watakuwa na kibarua cha kupambana na Mwadui FC kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi lakini waoka mikate hao wanafaida ya michezo miwili mkononi kutokana na kwenda Zambia kucheza mechi za kirafiki.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video