Hatimaye Gary Neville ameshinda mchezo wake wa kwanza baada ya kukosa ushindi ndani ya michezo mfululizo tangu akabidhiwe mikoba kama kocha wa Valencia. Valencia iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Espanyol.
Hata hivyo mapema tu kitumbua kiliingia mchanga baada ya makosa ya mlinda mlango wa Valencia Diego Alves ambayo yaliipa goli la uongozi Espanyol.
Lakini shukrani za pekee ziwaendee Alvaro Negredo na Denis Cheryshev ambao ndiyo walipeleka faraja kwa Neville baada ya kukosa ladha ya ushindi wa La Liga kwa takriban wiki 10.

Gary Neville akishangilia kwa uchu baada ya timu yake kuibuka na ushindi jana

Wachezaji wa Valencia Alvaro Negredo (kulia) na Denis Cheryshev wakishangilia baada ya kuipa ushindi wa mabao 2-1 timu yao dhidi ya Espanyol jana.
0 comments:
Post a Comment