Friday, December 11, 2015


Mbeya City fc kesho inashuka dimbani kucheza mchezo wa kwanza wa duru ya pili ya ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mtibwa Sugar ya Turiani Morogoro hii ikiwa ni mara ya tano kwa timu hizi kukutana katika kinyang’anyiro hiki.
Licha ya mchezo huu kuzikutanisha timu hizi kwa mara ya kwanza lakini ‘kipute’ kinaingia kwenye duru ya pili kufuatia kuchezwa baada ya kusimama kwa ligi kupisha usajili wa dirisha dogo na mechi za timu ya taifa.
Kocha wa City Abdul Mingange amesema yu tayari  kuikabili timu hiyo kutoka Turiani kwasababu ameshawaandaa vyema wachezaji wake kusaka matokeo hapo kesho.
“Niko tayari kwa mchezo wa kesho, nimewandaa vizuri vijana wangu kuhakikisha tunaibuka na ushindi, huu ni mchezo muhimu ambao tunahitaji kushinda ili kujijengea mazingira mazuri ya kupata matokeo kwenye michezo inayofuata, kumbuka baada ya hapa tutacheza na Mgambo kisha tutasafiri Dar kuikabiri Young Africans”…Amesema Mingange
Naye kocha wa Mtibwa Mecky Mexime ameumbia mtandao huu kuwa amekuja jijini hapa kufanya kazi, hivyo hana jambo lingine zaidi ya kusaka ushindi ili kuendelea kujikita katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi.
“Tumekuja kushinda, hatuna jambo lingine, kwetu sisi matokeo ni muhimu ili kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi” alijinasibu kocha huyo kijana.
Timu hizi zinakutana kwa mara ya tano, huku zikiwa na ushindi wa mara moja kila upande na sare mbili kila upande, lakini mara hii City ikiwa kwenye nafasi ya 11 na Mtibwa Sugar ikiwa nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video