Jose Mourinho amegoma kukanusha taarifa za Diego Costa kurejea Atletico Madrid, lakini ameendelea kushikilia msimamo kwamba mshambuliaji huyo ana furaha Chelsea.

'Atletico ni timu kubwa. Madrid ni mji mkubwa. La Liga ni ligi kubwa.
"Kwanini mchezaji mwenye umri wa miaka 27 asifikirie uwezekano wa kurudi huko? Sioni kama ni tatizo.

'Ana furaha hapa. Anapenda kuendelea kuwepo hapa. Nadhani ni miongoni mwa wachezaji ambao wataongeza miaka zaidi katika mikataba yao. Nadhani nitamuona akiendelea kukaa Chelsea kwa miaka mingine mitatu, sioni tatizo".Alisema Mourinho.
0 comments:
Post a Comment