
Raia huyo wa Wales mwenye umri wa miaka 44 atakuwa raia wa pili kutoka Wales kusimamia fainali baada ya Derek Bevan, aliyekuwa mwamuzi 1991 Australia walipoishinda England, katika uwanja wa Twickenham, ambao pia utakuwa mwenyeji wa fainali ya sasa.
Owens alisema kupitia mitandao ya kijamii kwamba anashukuru sana kutunukiwa hadhi hiyo.
New Zealand walicharaza Afrika Kusini 20-18 Jumamosi na watakutana na Australia, waliowashinda Argentina 29-15 Jumapili.
Mataifa hayo mawili hayajawahi kukutana kwenye fainali.
Mwingereza Ed Morrison, aliyekuwa refa fainali ya 1995 kati ya Afrika Kusini na New Zealand, na raia wa Ireland Alain Rolland, aliyesimamia fainali kati ya England na Afrika Kusini 2007, ndio marefa wengine kutoka kaskazini waliowahi kusimamia fainali ya dimba hilo.
Mwakilishi wa New Zealand jopo la kuteua refa wa kusimamia fainali Bw Grant Fox alikuwa tayari amedokeza kwamba Owens angesimamia mechi hiyo ya Oktoba 31 uwanjani Twickenham.
0 comments:
Post a Comment