Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza kikosi cha wachezaji 28 wa timu hiyo kitakachoingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Algeria wa kuwania kupangwa kwenye makundi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Urusi mwaka 2018.
Wachezaji wote walioitwa kwenye kikosi cha Stars walioitwa kwenye kikosi hicho, wanatakiwa kuripoti kwenye kambini Novemba 1 jioni kabla ya kuondoka kwenda Muscat, Oman kwa ajili ya kambi ya siku 11 kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria utakaopigwa Novemba 14 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Majina mapya kwenye kikosi hicho ni Elius Maguli, Hassan Kessy na Malimi Busungu wakati wachezaji ambao wameitwa tena baada ya kuwa nje ya timu hiyo ni Jonas Mkude, Salum Abubakar na Salim Mbonde.

Majina ya wachezaji wote (28) walioitwa kwenye timu ya taifa ni kama ifuatavyo;
Magolikipa:
1.Ally Mustafa (Yanga)
2. Aishi Manula (Azam)
3. Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
Walinzi wa pembeni:
1. Shomari Kapombe (Azam FC)
2. Mwinyi Haji (Yanga)
3. Mohamed Hussein (Simba)
4. Hassan Kessy (Simba)
4. Juma Abul (Yanga).
Walinzi wa kati:
1. Nadir Haroub
2. Kelvin Yondani (Yanga)
3. Salim Mbonde (Mtibwa)
4. Hassan Isihaka (Simba)
Viungo wa kati:
1. Himid Mao (Azam FC)
2. Mudathir Yahya (Azam FC)
3. Salum Abubakar (Azam FC)
4. Frank Domayo (Azam FC)
5. Said Ndemla (Azam FC)
6. Salum Telela (Yanga)
7. Jonas Mkude
Viungo wa pembeni:
1. Thomas Ulimwengu (TP Mazembe)
2. Farid Musa (Azam FC)
3. Mrisho Ngassa (Free State Stars)
Washambuliaji wa kati:
1. Mbwana Samatta (TP Mazembe)
2. John Bocco (Azam FC)
3. Elius Maguli (Stand United)
4. Malimi Busungu (Yanga)
5. Ibrahim Ajib
0 comments:
Post a Comment