Mabingwa wa kandanda Tanzania bara, Dar Young Africans leo jioni wameshinda 4-1 dhidi ya Kimondo katika mechi iliyopigwa uwanja wa CCM Vwawa Mbozi.
Kimondo walianza kwa kasi kubwa huku wakionesha kuuzoea uwanja wao.
Hadi kipindi cha kwanza kinaisha Kimondo walitoka kifua mbele kwa goli hilo moja,huku wakishangiliwa vilivyo na wakazi wa Mbozi.
Kipindi cha pili Yanga walirudi kwa ari mpya, kocha mkuu Hans van der Pluijm akiwaambia mastaa wake wakawafundishe soka wale vijana na ndipo Mvua ya magoli ikaanza.
Yanga wamehesabu magoli kupitia kwa:-
Geofrey Mwashiuya aliyefunga mawili.
Amiss Tambwe na Simon Msuva waliofunga moja moja.
Mapato yote ya mchezo huo yamechukuliwa na Kimondo FC.
0 comments:
Post a Comment