Wakati mabingwa wa kandanda Tanzania bara, Dar Young Africans wakiwa msituni mkoani Mbeya kujiandaa na mechi ya ngao ya jamii na ligi kuu soka Tanzania bara, miamba ya kandanda Afrika mashariki na kati, Azam fc iko chimbo visiwani Zanzibar.
Azam chini ya kocha mkuu, Muingereza, Stewart John Hall wanaendelea na mazoezi uwanja wa Amaan Zanzibar.
Yanga na Azam zitachuana Agosti 22 katika mechi ya Ngao ya Jamii kuashiria kufunuliwa kwa pazia la ligi kuu soka Tanzania bara.
Azam FC iliichapa Yanga penalti 5-3 katika mechi ya robo fainali ya kombe la Kagame, hivyo, Agosti 22 itakuwa siku ya kulipa kisasi, ingawa Wanalambalamba nao wanaonekana kuwa madhabuti.
Jana Yanga ilishinda 4-1 dhidi ya Kimondo FC katika mechi ya kirafiki iliyopigwa uwanja wa CCM Vwawa Mbozi.
0 comments:
Post a Comment