Arsene Wenger, kocha ambaye hapendwi sana na mashabiki wake kutokana na tabia yake ya kusajili kwa staili tofauti na klabu nyingine.
Licha ya kupoteza mchezo wa kwanza, Wenger bado ana imani kubwa na wachezaji wake.
Kwenye moja ya majibu aliyoyatoa kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu mechi iliyopita Wenger alisema, “Tunafanya kazi kwa bidii sana, tumejikita kuimarisha kikosi chetu tulichonacho. Ukipoteza mchezo unapata mawazo au hamu ya kusajili wachezaji wapya hasa kwa kipindi hiki. Lakini tungeweza kushinda ule mchezo bila ya kubadilisha kikosi kilichopo.”
Pia Wenger aliulizwa kuhusu tetesi nyingine ya timu yake kutaka kumsajili mchezaji Grzegorz Krychowiak kutoka Sevilla.
Bila kupindisha Wenger alijibu moja kwa moja 'Hapana'. Kwahiyo mchezaji huyo wa Sevilla kuanzia sasa ametoka kwenye orodha ya tetesi za kuelekea Arsenal.


0 comments:
Post a Comment