Miamba ya
kandanda nchini HISPANIA, FC BARCELONA na SEVILLA inakabiliana usiku huu katika
fainali ya UEFA SUPER CUP inayopigwa BORIS PAICHADZE DINAMO ARENA,
MJINI TBILISI, GEORGIA
Mchezo huu unaowakutanisha
Mabingwa wa UEFA CHAMPIONZ LIGI na waliobeba UEFA EUROPA LIGI, ndio unaoashiria
kuanza rasmi kwa Msimu mpya wa Soka Barani Ulaya.
Mechi hii ya kusisimua inaanza
kupigwa kuanzia Saa 3 Dakika 45 Usiku huu kwa saa za Afrika mashariki.
FC Barcelona
wanatinga Uwanjani bila ya nyota wake wa Brazil Neymar, huku wakisaka kuifikia rekodi ya AC Milan ya
kutwaa mara tano UEFA Super Cup.
Mbali ya kumkosa Neymar, ambaye
nafasi yake inachukuliwa na Pedro anayedaiwa kuhamia Manchester United baada ya
Mechi hii, Barca, chini ya Kocha Luis Enrique, pia inawakosa majeruhi Jordi
Alba na Douglas.
Wachezaji wapya, Arda Turan na Aleix Vidal hawaruhusiwi kucheza
hadi Januari kwa vile hivi sasa Barca ipo kwenye Kifungo cha FIFA cha
kutosajili.
Hii ni
mara ya pili mfululizo kwa Sevilla kugombea UEFA Super Cup baada ya kutetea vyema
Taji lao la EUROPA LIGI lakini Mwaka Jana kwenye Fainali hii walichapwa magoli
mawili kwa bila dhidi ya Real Madrid.
Sevilla,
chini ya Kocha Unai Emery, hawajaifunga Barcelona katika Mechi 19 ingawa safari
hii wana nguvu mpya ya Wachezaji wapya , YEVHEN KONOPLYANKA na CIRO IMMOBILE.


0 comments:
Post a Comment