Tuesday, August 11, 2015

mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesikia ushindi wa Simba kwenye michezo sita ya kirafiki huku akifuatilia rekodi za straika Hamis Kiiza na kutamka kuwa kama hatapewa ushirikiano ni lazima achemshe Msimbazi.
Akizungumza na Mwanaspoti, Niyonzima aliyewahi kucheza na Kiiza ndani ya Yanga, alisema straika huyo anapata wakati mgumu sasa kutokana na kubadili mazingira na itachukua muda kuyazoea, hivyo ni lazima Simba impe muda kabla ya kuanza kumhukumu.
“Kiiza ameenda Simba, huenda akapata tabu ya kuendana na staili ya uchezaji wa Simba na kama akinyimwa ushirikiano atapotea kabisa.
“Simba na Yanga zina falsafa tofauti ingawa mchezaji yeyote mzuri ataweza kuendana na mpira wowote ule, cha msingi ushirikiano na kama hilo litakuwepo, mtu kama Kiiza ataweza kutamba lakini kama hali itakuwa tofauti, itamchukia na hatoweza kutamba,” alisema.
Alisema lazima Kiiza apate mawinga wenye kasi, pia anahitaji timu impe nafasi ya kufanya yake na kama timu itapiga pasi nyingi za taratibu mambo huenda yakawa magumu kwake.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video