Wiki za karibuni kumekuwepo na tetesi nyingi zinazomuhusisha Winga kinda wa Manchester United, Adnan Januzaj kujiunga na klabu ya Sunderland.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye miaka 20, leo amekanusha tetesi hizo kwa tweet ya neno moja tu ambalo linaashiria haendi popote majira haya ya kiangazi.
Januzaj alianza katika mechi saba tu msimu uliopita chini ya Louis van Gaal, lakini alitumika pia katika maandalizi ya msimu mpya ambao tayari umeanza kutimua vumbi.
Sunderland ambao walifungwa 4-2 na Leicester City katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ya England mwishoni mwa Juma lililopita bado wanatafuta wachezaji wapya.
Adnan Januzaj hakupangwa kabisa katika kikosi cha Manchester United kilichocheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Tottenham na kuibua tetesi kuwa anakwenda Sunderland kwa mkopo.


0 comments:
Post a Comment