Mamlaka ya Kodi na Mapato nchini (TRA) Ijumaa ya Agosti 14 inatarajia kuendesha semina ya kodi kwa viongozi wa klabu zilizopo jijini Dar es salaam katika hoteli ya Tiffany iliyopo eneo la Kisutu.
TRA itaendesha semina hiyo kwa klabu za ligi kuu, ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili ambapo viongozi wakuu wa klabu hizo, Katibu Mkuu, Mwenyekiti, na Mhasibu wanapaswa kuhudhuria semina hiyo.
Kwa kuanzia TRA itaendesha semina hiyo jijini Dar es salaa, na baadae kuendelea na semina hizo kwa klabu zilizopo mikoani kwa lengo la viongozi wa klabu kutambua umuhimu wa ulipaji kodi kwa wachezaji, makocha wanaowaajiri katika vilabu vyao.
Semina hiyo itaanza saa 3 asubuhi mpaka saa 5 kamili asubuhi katika hoteli ya Tiffany iliyopo eneo la Kisutu jijini Dar es salaam, vionggozi wa vilabu vya ligi kuu, ligi daraja la kwanza, ligi daraja la pili waliopo jijini Dar es salaam mnaombwa kuhudhuria semina hiyo.


0 comments:
Post a Comment