Washika bunduki wa London, Arsenal wameshinda 2-1 dhidi Crystal Palace katika mechi ya ligi kuu England iliyomalizika jioni hii uwanja wa Selhurst Park.

Arsenal walikuwa wa kwanza kuandika goli dakika ya 16' kupitia kwa Olivier Giroud, kabla ya Joel Ward kuwasawazishia wenyeji dakika ya 28.

Damien
Delaney alijifunga dakika ya 55 na kukipa ushindi kikosi cha Arsene Wenger ambacho kilifumuliwa 2-0 dhidi ya West Ham United kwenye mechi ya ufunguzi wa EPL iliyochezwa mwishoni mwa Juma lililopita.
TAKWIMU ZA MECHI
Baada ya mechi hiyo msimamo wa sasa hivi uko hivi;

0 comments:
Post a Comment