Kituo cha Television cha Azam Media Limited leo kimezindua Channel mpya maalumu kawa ajili ya kuonesha michezo, channel hiyo iliyopewa jina la Azam Sports HD imezinduliwa kwa ajili ya kuonesha ligi kuu ya Hispania maarufu kama La Liga lakini itaonesha ligi kuu Tanzania bara (VPL) pamoja na michezo mingine mingi kama mbio za magari, riadha, kuogelea na basketball.
Mtendaji mkuu wa Azam Media Limited Rhys Torrington akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa channel mpya ya michezo
Mtendaji mkuu wa Azam Media Limited Rhys Torrington amesema lengo la kuanzisha channel hiyo ni kuhakikisha watazamaji wa Azam TV hasa wapenda michezo wanapata fursa ya kutazama ligi kuu ya Hispania pamoja na VPL lakini bila kusahau michezo mingine ukiondoa soka.
Torringson ameongeza kuwa, mbali na kupata fursa ya kuangalia michezo kwenye channel inayojitegemea, watazamaji wataona picha ambazo ni ang’avu (HD) na zenye ubora wa hali ya juu kupitia channel hiyo.
Vijana wakionesha baadhi ya jezi ambazo huvaliwa na timu zitakazokuwa zinaonekana kupitia Azam Sports HD
Kwa upande wa naibu mtendaji mkuu wa Azam Media Limited Bw. Tido Mhando yeye amesema mbali na watazamaji kutazama picha ang’avu, watapata fursa ya kupata uchambuzi na matangazo ya moja kwa moja kwa lugha ya Kiswaili kutoka wa watangazaji wa michezo wa kituo hicho.
Mtangazaji mkongwe wa Tanzania ambaye alikuwa akitangaza kwa Kiswahili kwenye Shirika la Utangazaji nchini Uingereza Charles Hilary amesema yeye pamoja na timu yake nzima ya watangazaji wa habari za michezo wa kituo hicho wamejipanga kuhakikisha watazamaji wanapata burudani kupitia channel hiyo mpya ya michezo.
Hilary akiwa ndiye kiongoi wa timu ya watangazaji wa michezo pamoja na wachambuzi, amekitaja kikosi anachokiongoza kinachoundwa na watangazaji na wachambuzi wafuatao;
Watangazaji
1. Charles Hilary
2. Baruani Mhuza
3. Patrick Nyembelan
4. Philipo Cyprian
5. Twalib Omary
6. Ahmed Abdallah
7. Rehema Jarufu
8. Sheiza Mungilwa
9. Michael Maluwe
Wachambuzi
1. Eddo Kumwembe
2. Ally Mayay
3. Jeff Lea
4. Kally Ongala
5. Hussein Sappi







0 comments:
Post a Comment