Walcott (kushoto) akiteta na Petr Cech
Theo Walcott ana uhakika wa kubakia Arsenal akitabiri kwamba mazungumzo ya kuongeza mkataba hayatachukua muda mrefu.
Kufuatia kuondoka kwa Abou Diaby majira haya ya kiangazi, Walcott amekuwa nguzo ya timu na ripoti ya Telegraph inasema kwamba straika huyo yupo katika hatua ya mwisho ya mazungumzo ya kuongeza mkataba.
Walcott ambaye alijiunga na Arsenal mwaka 2006 akiwa na umri wa miaka 16, baada ya kufunga goli katika fainali ya FC mwezi Mei mwaka huu ambapo Arsenal walichukua ubingwa, anajipanga kupata mafanikio zaidi msimu ujao.
"Wakala wangu amezungumza na klabu, nafurahia kucheza klabuni hapa, hivyo nimewaacha wamalizane. Nitaendelea kucheza mpira hapa". Amesema Walcott.
"Acha tusubiri tuone mambo yatakwendaje, lakini nina uhakika haitachukua muda mrefu. Kwangu mimi kikosi hiki ndio bora zaidi, nataka kuendelea kuwa sehemu yake".
Mkataba wa sasa wa nyota huyo wa kimataifa wa England unamalizika majira ya kiangazi mwakani na mazungumzo ya kuongeza yanaendelea.
Walcott na kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, wote wanaamini kuwa imefika wakati wa mchezaji huyo kutimiza malengo ya klabu.
Miezi 18 iliyopita Theo Walcott alisaini mkataba unaomlipa mshahara wa paundi 90 kwa Juma na sasa anajiona kama anastahili kulipwa paundi laki moja.
0 comments:
Post a Comment