Robin van Persie amejibu mapigo kwa kocha wake wa zamani Louis van Gaal, baada ya kutompa nafasi ya kuthibitisha utayari wake kwa ajili ya mapambano mapya katika klabu ya Manchester United.
“Hiyo ilikuwa ni ishara ya kwanza kwamba mambo yalikuwa hayaendi kama ilivyotakiwa”, aliliambia gazeti la the Sunday Times.
“Nilimuomba kucheza nikitokea benchi, ili nirudishe kasi yangu ya awali, lakini baada ya hapo niliendelea kuwekwa bechi tena. Hali ilibadilika kati yangu na Louis na hata baadhi ya watu kwenye timu waliona hilo, lakini mara zote nilikuwa mweledi. kwa wakati huo sikuwa nimefikiria kuondoka. [Mke wa Van Persie] Bouchra alikuwa na furaha tu. watoto walikuwa na furaha katika jiji la Manchester.
“Lakini hata hivyo bado nilikuwa na fikra ya kwamba nikirudi kutoka mapumzikoni tutaanza mambo upya. Alikwisha badili maamuzi yake kuhusu mimi tangu hapo kabla. Wakati alipoanza kuifundisha Uholanzi aliwahi kuniambia kwamba‘Wewe ni mshambuliaji chaguo la tatu hapa.’ Nikasema sio tatizo’ Lakini nilipambana na baadaye kuwa chaguo la kwanza na nahodha wake pia.
“Lakini wakati niliporudi, Hakukuwa na uhalisia wa kile kilichokuwa kikiendelea. Kupambana ili kurejea katika kikosi cha kwanza haikuwa ombi bali ni lazima kwangu. Alinipeleka kwenye kikosi cha pili. Na mimi ni mchezaji niliyekwisha pevuka tayari. Sio mpuuzi mimi. Kamwe siku na hasira wala jazba. Haya mambo ni sehemu ya mchezo, sehemu ya maisha. lazima ufanye maamuzi sahihi katika wakati wowote ule, hivyo basi nafanya hili ili nisonge mbele.
“Namjua Louis kama kocha wa timu ya taifa na sasa namjua kama kocha wa klabu. N awkati huo huo kumbe kuna utaofauti mkubwa”.
0 comments:
Post a Comment