Kenedy (kulia) akichuana na Cesc Fabregas
Nyota kinda wa Brazil, Kenedy ni miongoni mwa wachezaji 24 wa Chelsea waliofanya mazoezi jana mjini Montreal, Marekani.
Chelsea chini ya kocha Jose Mourinho imeanza kutafuta kasi ya kutetea ubingwa wake wa ligi kuu England msimu ujao.
Katika mazoezi ya jana, Kenedy aliongezwa katika kundi la wachezaji wa kikosi cha kwanza na tayari klabu yake ya Fluminese ya Brazil imemruhusu kijana huyo mwenye miaka 19 kujiunga na machampion wa EPL.
Ada ya uhamisho wake kutua Stamford Bridge itakuwa paundi milioni 6.3

Kenedy (kulia) akiongozana na Wabrazil wenzakeRamires na Diego Costa baada ya mazoezi


Diego Costa akipiga matizi

Jose Mourinho akiwapa maelekezo vijana wake 24 kwenye mazoezi yaliyofanyika jana Montreal Impact Training Centre

Mlinzi raia wa Serbia, Branislav Ivanovic akipiga selfie na mashabiki wawili

Nahodha, John Terry naye kama kawaida
0 comments:
Post a Comment