Friday, July 3, 2015




Mechi kati ya Taifa Stars na The Cranes( Uganda) itapigwa ndani ya jiji la Kampala jumamosi hii majira ya Saa kumi kamili jioni katika ule uwanja maarufu sana nchini Ugana na Afrika mashariki kwa ujumla. Uwanja wa Nakivubo.
  Nakivubo unapatikana ndani ya jiji la Kampla katika wilaya ya Kampala inayo karibiana na soko kuu la Balikuddembe.
  Ni mitaa mikubwa yenye pilika nyingi za kibiashara.
  Lakini uwanja huo haushi vituko na kadhia za hapa na pale.
  Mwaka 2011 ulifungiwa na mamlaka ya mapato ya Uganda kwa madeni lakini ndani ya wiki moja ulifunguliwa kabla ya kufungiwa tena mwaka 2013 pia kwa madeni ya kodi .
  URA waliufungua tena mwaka jana (2014) na kuanza kutumika upya.
  Nakivubo unatumika kama uwanja wa nyumbani wa klabu kongwe ya SC Villa na timu zote za taifa za nchi hiyo. Wapinzani wakubwa wa Villa ambao ni The Express wenyewe wana miliki uwanja wao " Mutessa 2nd".
  Nakivubo ndicho kiwanja kikubwa zaidi Afrika mashariki kikiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 140,000 .
  Taifa Stars iliyotinga jana nchini Uganda , inatarajiwa kupewa sapoti kubwa na kundi kubwa la Watanzania ambao wameondoka alfajiri ya leo na mabasi kuelekea Uganda.
Kundi hilo linajulikana kama Taifa Stars Supporters lilipata baraka zote jana na mwenyekiti wa TFF ndugu Jamali Malinzi akiwakabidhi motisha ya jezi , fedha za kujikimu njiani na huko Kampala katika ile kutambua thamani ya uzalendo wao kujitoa kuipa sapoti timu yao.
  Kundi hilo lenye zaidi ya watu 100 wanakwenda nchini humo kwa gharama zao za usafiri licha ya motisha hiyo toka TFF hii inaonesha mipango, itikadi na sera nzuri zikiwekwa , watanzania bado wana uzalendo mkubwa na rasilimali zao ikiwemo timu hiyo.
  Viongozi wanao ambatana na kundi hilo ni Mwenyekiti ndugu Madaraka Marumbo, Yusuphed Mhandeni, Maulidi Kitenge, Kaisi, Sekamba, Angelo, Carlos Leonard, Ziota Musisa na mratibu wa kundi hilo Josephat Sinzobakilwa.
   Ikumbukwe mechi ya kwanza mjini Zanzibar , Stars ilifungwa 3_0 hivyo wanahitaji ushindi wa 4_0 ili timu hiyo isonge mbele.

Samuel Samuel in sports ikiongea na mdau mkubwa wa timu hiyo aliyeko safarini ndugu Salumu Mbalale alitanabaisha
   " tuna imani kubwa na Mungu wetu , ushindi upo Kampala ndio maana sisi tumeweka silaha chini na kusafiri safari ndefu kama hii kupitia Nairobi hadi Kampala kwa sababu tunajua korongo anakaa"
  Samuel Samuel in sports inawatakia safari njema wazalendo hao na pia ushindi mnono kwa taifa stars.
  Mungu ibariki Afrika , Mungu ibariki Tanzania.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video