Gazeti la mji wa Valencia, Superdeporte leo limekuja tena na ripoti katika ukurasa wake wa mbele likimzungumzia Mlinzi wa Argentina, Nicolas Otamendi (tazama picha juu).
Gazeti hilo linaripoti kwamba Manchester United na Manchester City zitaweka mezani ofa ya kumsajili mlinzi huyo wa kati wa Valencia, ingawa limeshindwa kutaja kiasi ambacho kila klabu itaweka.
klabu inayotakiwa kumsajili Otamendi, inatakiwa kulipa Euro milioni 50 na Valencia wamekomaa na dau hilo.
Haifahamiki kama Manchester United na Man City zitatuma ofa wiki hii, ingawa Superdeporte linafafanua kwamba klabu hizo zimemwambia kuwa zitamlipa mshahara wa Euro milioni 3.5 mpaka 4 kwa mwaka.
Zaidi, gazeti hili linaripoti kwamba klabu zote mbili zimeshakaa na wakala wa mchezaji, Jorge Mendes kujadili uwezekano wa kumsajili Otamendi na Mikutano yote imefanyika, Mjini Porto, Ureno.
0 comments:
Post a Comment