Kutoka katika ukurasa maarufu wa facebook wa 'Naipenda Yanga' kuna taarifa kuwa, klabu ya Yanga ipo katika hatua za mwisho kumsajili mshambuliaji wa kutegemewa wa Gor Mahia na mfungaji bora wa KPL Michael Olunga
Inaelezwa kuwa makubaliano ya awali baina ya mchezaji na klabu yamefikiwa huku Yusuf Manji akisisitiza lazima Mkenya huyo atue Jangwani baada ya kuvutiwa mno na soka lake.
Ikumbukwe Olunga aliisumbua mno safu ya Ulinzi ya Yanga na kuweza kufunga goli la pili katika ushindi wa 2 - 1 walioupata K'ogallo.
Wakati huo, Uongozi wa Simba kupitia kwa mwenyekiti wake wa kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe umethibitisha kuanza mazungumzo na Olunga ili kumsajili.
Wakati huo, Uongozi wa Simba kupitia kwa mwenyekiti wake wa kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe umethibitisha kuanza mazungumzo na Olunga ili kumsajili.
0 comments:
Post a Comment