KOCHA Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, ameonyesha kuumizwa mno kwa kipigo walichokipata Yanga kutoka kwa Gor Mahia ya Kenya, huku akimtupia lawama mshambuliaji wa watani wao hao wa jadi, Donald Ngoma kwa kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 25 na hivyo kuivuruga timu yake.
Ngoma alionyeshwa kadi hiyo katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo katika michuano ya Kombe la Kagame kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, baada ya kumpiga beki wa Gor Mahia, Haruna Shikanda.
Kerr alitinga uwanjani hapo kuangalia mchezo huo ambapo alitumia dakika zote 90 kuwasoma Yanga, kuanzia mifumo yao, ubora, udhaifu wa timu na mchezaji mmoja mmoja.
Chanzo:Bingwa
0 comments:
Post a Comment