Wasanii wa sanaa za maigizo maarufu kama ‘Bongo Movies’ wanaoishabikia klabu ya Simba leo wamekabidhiwa kadi za uanachama wa klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuelekea kwenye kilele cha siku ya Simba ijulikanayo kama ‘Simba Day’ ambayo huadhimishwa kila ifikapo Agosti 8 kila mwaka.
Mwenyekiti wa klabu hiyo Evans Aveva ndiye aliyewakabidhi kadi hizo wasanii wakiongozwa na Jacob Steven ‘JB’, Mtitu, Monalisa pamoja na Odama ambao wote kwa pamoja wakekuwa wanachama wapya wa klabu hiyo kuanzia sasa.

“Simba ni klabu kubwa iliyojaa historia ya aina yake na mimi najivunia kuwa mwanachama wa klabu hii japo timu yetu imekuwa haifanyi vizuri sana kwa siku za hivi karibuni”, amesema JB.

Katika hatua nyingine, Simba imesema imeialika timu ya FC Leopards kuja kucheza mchezo wa kirafiki katika kusherehekea siku ya Simba Day itakayoadhimishwa Agosti 8 mwaka huu. Rais wa Simba Bw. Aveva ameongeza kuwa, siku hiyo kutakuwa na mechi ya utangulizi kati ya viongozi wa Simba watakao kipiga dhidi ya wasanii wa Bongo Movies kabla ya mtanange wa Simba SC dhidi ya FC Leopard.
0 comments:
Post a Comment