Raheem Sterling baada ya kusajiliwa kwa pesa nyingi (paundi milioni 49) akitokea Liverpool na kujiunga na matajiri manchester city anategemewa kuanza kucheza.
Hivi sasa Raheem yupo pamoja na wachezaji wenzake kwenye mazoezi chini ya kocha Manuel Pellegrini na meneja huyo amesema mechi ya kwanza ya Sterling ni dhidi ya Roma inayopigwa leo hii.
Mashabiki wa Manchester city wanategemea kumuona mchezaji huyu akitoa mchango mkubwa kwenye club yao baada ya mambo makubwa aliyokua akifanya ndani ya Liverpool .Raheem amepewa jezi namba 7
0 comments:
Post a Comment