Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
MFUNGAJI Bora wa zamani wa Yanga, Mkenya Boniface Ambani, ameipa mbinu Gor Mahia kuiua timu hiyo ya Jangwani katika mechi yao ya leo ya ufunguzi wa Kombe la Kagame kwenye Uwanja wa Taifa jijini hapa.
Ambani, ambaye alikuwapo Dar es Salaam wakati Yanga ikiikung'uta mabao 3-0 Kombaini ya Polisi, amesema mabingwa hao wa Tanzania wana udhaifu mkubwa kwenye safu yao ya ulinzi na ameitaka Gor Mahia kutumia udhaifu huo kupata ushindi leo.
"Yanga ina tatizo kubwa kwenye safu ya ulinzi kutokana na kutokuwa na mabeki wengi wa maana. Hata waliopo wamechoka maana hawajapumzika tangu kumalizika kwa ligi. Hii ni nafasi nzuri kwa Gor Mahia kutumia udhaifu huo," amesema Ambani.
0 comments:
Post a Comment