Friday, June 12, 2015


Shabani Kado akipokea tuzo yake ya golikipa bora wa msimu uliomalizika

Tuzo ya mlinda mlango bora wa ligi kuu msimu wa 2014/2015 imetua mikononi mwa Shabani Kado golikipa wa zamani wa Coastal Union, Mtibwa Sugar na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’. 
Kado ambaye kwa sasa amesajiliwa na Mwadui FC, alipokea tuzo hiyo jana usiku kwa kuwabwaga magolikipa wengine wawili Mohamed Yusuph (Tanzania Prisons) na Said Mohamed (Mtibwa Sugar).
Baada ya Shabani Kado kuibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro hicho, golikipa huyo amesema anamshukuru Mungu kwa kumuwezesha kuibuka mshindi wa tuzo hiyo huku akitoa ahadi ya kutetea tuzo hiyo kwa msimu ujao akiwa na timu yake mpya ya Mwadui FC ya mjini Shinyanga.
“Kwasababu ukiangalia kipa bora nilichukua msimu wa 2008-2009 nikiwa Mtibwa kwahiyo nashukuru Mungu. Nafikiri katika watu waliokuwa wanaangalia performance wameona kitu kwasababu mpaka napewa nafasi hii kuna kitu mtu kaona, namshukuru Munu kwa hili”, amesema Kado golikipa bora wa msimu uliomalizika.
“Ukiaangalia kwenye timu niliyotokea toka nimeenda pale mimi nimekuwa msaada mkubwa sana katika timu, na hilo nalo linaweza kuwa limechangia mimi kupata nafasi hii, kwasasa nipo Mwadui FC kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu  naweza nikafanya kile nilichokifanya nikiwa Coastal Union. Mwalimu anayenitrain Mwadui ni yuleyule ambaye alikuwa Coastal, kwahiyo ninauhakika nitamaintain performance”, Kado alimaza.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video