Dkt. Jonas Tiboroha katibu mkuu wa klabu ya Yanga
Kufuatia jiana la kocha msaidizi wa Yanga Charles Boniface Mkwasa kutajwa kuirithi mikoba ya Mart Nooij aliyetimuliwa, uongozi wa Yanga umevunja ukimya na kuamua kutoa kauli juu ya kocha huyo mzalendo ambaye anamsaidia Hans van der Pluijm kukinoa kikosi cha Yanga kama kuna uwezekano wowote wa kumwachia ili akajiunge na timu ya Taifa.
Katibu mkuu wa klabu ya Yanga Dkt. Jonas Tiboroha amesema, Yanga bado inamuhitaji sana Mkwasa kwa ajili ya maendeleo yake ya soka na kama watamruhusu kocha huyo kuifundisha timu ya Taifa basi itakuwa ni kwa muda tu lakini sio kwa muda wote kwa sababu Mkwasa bado ana mkataba wa kuifundisha Yanga.
“Mimi kwa kujibu harakaharaka tu japokuwa najua sijawasiliana na viongozi wenzangu kuhusu hilo wala mwalimu mwenyewe hajaniambia hicho kitu lakini watu lazima wakumbuke kwamba Charles Boniface Mkwasa anamkataba na Yanga na kwa maana hiyo lazima uwepo muafaka kati ya Yanga na TFF utakaofanya Yanga imruhusu Boniface kitu ambacho pia nakiona kigumu labda kama itakuwa ni kwenye ‘part time engagement’”, amesema Tiboroha.
“Lakini on full time basis siioni hiyo kutokea sasa hivi kwa sababu huyu bado ana mkataba wa kuifundisha Yanga na mkataba wake haushi kesho. Unajua mambo mengi sana tunataka kuyabadilisha kwa kutumia mbinu ya ‘kitaifa’, ndio maana tumesema Yanga tunaweza tukamruhusu on part time basis lakini sio full time”, ameeleza.
“Na yeye pia ni mwajiriwa wa Yanga kwa maana hiyo taifa pia lazima liangalie kwamba maendeleo ya mpira nchini sio timu ya taifa tu, hasa ingetakiwa Mkwasa afanye kazi kubwa sana Yanga ili atengeneze wachezaji watakaoenda kuchezea timu ya taifa badae”, amefafanua.
“Kiala mtu anajua Mkwasa ni kocha mzuri sana, ni moja ya makocha bora sana nchini, kocha ambaye kwakweli huwezi kumpata kirahisi kataka nchi hii, kwa maana hiyo Yanga inabahati sana kuwa na kocha kama huyu na ndiyo maana nasema sidhani kama klabu itakuwa iko tayari kuachana nae sasahivi kwasababu ni kipindi ambacho inamuhitaji sana kwenye mipango yake ya maendeleo”, alimaliza Tiboroha.
Jina la Mkwasa ndiyo jina pekee ambalo limekuwa likitajwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Mholanzi Mart Nooij aliyesitishiwa mkataba wake kuanzia tarehe 21 May (jana) kutonana na mwendelezo wa matokeo mabovu ya timu ya Taifa kwenye michuano mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment