Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Kocha mkuu wa Mbeya City FC, Juma Mwambusi, amesema kuwa ana imani kubwa na wachezaji nyota walio katika timu ya vijana ya City U20 akitumaini watakuja kuleta mafanikio makubwa kwa timu yao siku za usoni.
Akizungumza mapema leo Mwambusi anayejulikana kwa kuibua vipaji na kuviendeleza, amesema kuwa ubora wa wachezaji vijana walio katika timu hiyo ya U20 umempa imani kubwa kuwa City itakuwa timu bora zaidi kwenye ligi kuu siku zijazo ikiwa inatumia wachezaji wa ndani.
“Vijana wetu walikuwa na ziara ya michezo 8 ya kirafiki huko Sumbawanga, wameshinda mechi 6, kupoteza mmoja na sare moja, hii ni taswira nzuri kwa timu yetu, ukiwa na wachezaji wanaoweza kupambana na kukupa matokeo kwenye mechi sita mfululizo unakuwa na imani kubwa, tutaendelea kuwajenga ili wazidi kuwa bora tayari kwa kuitumikia City kwa mafanikio," amekaririwa Mwambusi katika mtandao rasmi wa City leo.
0 comments:
Post a Comment