BAADA ya kumnasa Jackson Mayanja, Coastal Union wamemwajiri Mganda mwingine baada ya leo kumpa mkataba wa miaka miwili kocha wa makipa Fred Lumu kutoka klabu ya KCCA ya Uganda pia.
Oscar Assenga, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Coastal Union, amesema leo kuwa wameamua kumwajiri kocha huyo mwenye Lesini C ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) ili kuimarisha benchi lao la ufundi.
"Lumu ameahidi kuimarisha makipa wetu ili wawe muhimili imara katika kuipa timu mafanikio," amesema Assenga.
Lumu anaungana na Mganda mwenzake, Mayanja ambaye jana alimwaga wino kuwatumikia kwa miaka miwili mabingwa hao wa Tanzania Bara 1988.
0 comments:
Post a Comment