Friday, June 12, 2015

NDANDA FC imelazimika kuongeza utulivu katika kipindi hiki cha usajili ili kupata wachezaji wataoifanya kuwa timu tishio msimu wa 2015/2016 wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Kaimu katibu mkuu wa Ndanda, Seleman Kachele amesema wapo wachezaji wengi waliopo kwenye rada zao na wanawaangalia kwa jicho la kitaalamu.
“Wachezaji wapo wengi, sisi hatusajili majina ya wachezaji, tunasajili kwa kitaalamu na tunaamini tutakuwa na wachezaji wazuri wataoifanya timu iwe vizuri. Tumekuwa na utulivu, tuko hatua za mwisho mwisho, tukikamilisha tutawatangazia. Tunaweza kusajili wachezaji wa nje ya Tanzania au hapa hapa nchini kutegemea na matakwa ya mwalimu”. Amesema Kachele.
Kachele ameweka wazi kwamba ripoti ya mwalimu aliyemaliza mkataba na klabu hiyo, Meja Mstaafu, Abdul Mingange imebainisha mapungufu kadhaa yaliyojitokeza msimu uliopita.

“Mingange katika ripoti yake amesema mapungufu yapo kwenye kikosi, anataka wachezaji wengine kama mabeki wa pembeni, kulia na kushoto, mabeki wa kati, golikipa na kiungo mchezeshaji”. Amesema Kachele na kuongeza: “ Kocha mpya Jumanne Chale ataangalia hayo na kuongezea yakwake, lakini sisi hatuwezi kusajili mchezaji wa kimataifa mwenye uwezo sawa na mchezaji wa hapa mjini”.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video