Klabu ya ‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba imethibitisha rasmi kutoshiriki michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kagame Cup itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia mwezi Julai kufuatia kutopata barua ya mwaliko wa kushiriki michuano hiyo kutoka kwa baraza la vyama vya soka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
“Mashindano ya Kagame sisi hatushiriki, klabu ya Simba haishiriki mashindano ya Kagame. Hatujaalikwa hatujapata taarifa ya kutoshiriki, hatushiriki wala hatujaalikwa, hatumo kabisa kwenye mashindano ya kagame. Sio kwamba tumepewa taarifa ya kutoshiriki, hatujapewa taarifa ya kushiki”, amesema Manara.
Unajua mazoezi inategemea na mipango ya mwalimu, mwalimu wetu mpya anataka kwa uchache angalau apate wiki sita kabla ya ligi kuanza. Hatuwezi kushiriki kwasasa mashindano ya Kagame wakati barua hatujapewa, ilikuwa ni vigumu sana, na Kagame tumeambiwa inaanza Julai hapa katikati sasa huwezi kwenda kucheza Kagame wakati timu haijaandaliwa”, amefafanua.
“Sisi tunaingia ‘camp’ tarehe 1 Julai kuanza mazoezi ya maandalizi kwa ajili ya msimu ujao huko tutakapokuwa, nadhani tutakuja hapa Dar es Salaam siku chache kabla ya siku yetu ya Simba day. Lakini mazoezi mepesi nadhani wiki hii tunatarajia kuanza, wapi, siku gani, nitawajulisha Jumatatu kwenye mkutano wetu na waandihi wa habari”, ameeleza msemaji wa Simba.
Awali klabu ya Simba ilisema inasubiri kama itapata mwaliko wa kushiriki michuno hiyo lakini inavyoonekana mambo yamekwenda kinyume na walivyotarajia. Timu zenye nafasi ya kushiriki michuano hiyo ni bingwa wa ligi wa nchi husika na timu ambayo imemaliza ikiwa nafasi ya pili, lakini nchi mwenyeji huwa inapewa nafasi moja ya upendeleo na nafasi hiyo huenda kwa mshindi wa tatu kwenye ligi.
Simba inakosa vigezo hivyo kutokana na kumaliza ikiwa nafasi ya nne kwenye ligi ya msimu wa 2013-2014 huku Azam ikimaliza kama bingwa wa ligi wakati nafasi ya pili ikienda kwa Yanga na nafasi ya tatu ikachukuliwa na Mbeya.
0 comments:
Post a Comment