COPA AMERIKA 2015
MAHALI: MAJIJI 8 YA CHILE
TAREHE: 11 JUNI – 04 JULAI
TAREHE: 11 JUNI – 04 JULAI
Hadi itakapo fika tarehe 4 mwezi Julai, mataifa 10 ya bara la Amerika ya kusini pamoja na wageni waalikwa, Mexico na Jamaica watakua wakipambana katika fainali za 44 za bara hilo.
1)Ni chimbuko la nyota wengi duniani
Louis Suarez bado anatumikia adhabu yake aliyofungiwa na FIFA lakini wachezaji wenzake wa Barcelona Neymar na Lionel Messi wako tayari kung’arisha radha ya mashindano hayo makubwa kabisa barani humo. Sergio Aguero sambamba na nyota wa Manchester United, Angel Dimaria wote wako hapa.

Nyota wa Real Madrid, James Rodriguez pamoja na Muuruguay Edson Cavani wanafanya mashindano haya kuwa si ya kukosa kuyatizama.
2)Historia
Copa Amerika ndio michuano mikongwe zaidi ya mabara duniani. Ilianza mwaka 1916. Awali ilifanyika kila mwisho wa mwaka na baadae ikajitangaza na kuwa sababu ya uandaaji wa kombe la dunia 2030.

3)Imeshiba
Michuano hii inajitosheleza na imekua ikizaa matunda kwa timu za taifa za ukanda huu, kwa mfano Uruguay walikua vizuri sana katika kombe la dunia la 2010 Afrika Kusini wakati Colombia wakitesa katika fainali zilizopita. Timu hizi kutoka ukanda huu ni nadra sana kutolewa hatua za awali za michuano ya kombe la dunia.

4)Haitabiliki (Unpredictably)
Copa America 2015
Copa America 2015
Kundi A Kundi B Kundi C
Chile Argentina Brazil
Mexico Uruguay Colombia
Ecuador Paraguay Peru
Bolivia Jamaica Venezuela
Timu 8 kati ya 12 zitafuzu kucheza mtoano huku kukiwa hakuna muda wa nyongeza katika michezo. Bara hili lina historia ya kuibuka kwa timu yenye uwezo wa chini na kufanya maajabu.
5)Idadi nzuri ya timu kwenye mashindano
Kombe la dunia lina timu 32 wakati michuano ya bara la Ulaya ina timu 16. Amerika kusini wao wanakua na timu 12 tu na hivo ni rahisi kuziongoza na inaleta ugumu wa mashindano.

6)Presha ya top 3
Pamoja na uwepo wa makundi 3 katika michuano hii, lakini bado kuna timu zenye historia na michuano hii. Brazil, Argentina na wenyeji Chile wanafanya timu hizi kuwa katika presha kubwa ya kufanya vizuri. Presha hii inaongezeka kutokana na uwepo wa timu kama Uruguay, Colombia na Ecuador ambazo zinaweza kutibua wakubwa kufanya wanayotarajia.

7)Usawa katika ushambuliaji
Kawaida mashindano yeyote huwa na kitu cha tofauti, lakini kitu cha upekee katika Copa Amerika ni timu nyingi kuwa na washambuliaji wa kiwango cha dunia.

Huku kuna Neymar, kule Messi, hapa Cavani…. Ni michuano ya kuvutia.
8)Mashabiki
Zamani Amerika Kusini kulikua na askari wengi kuliko washangiliaji. Hali ni tofauti hivi sasa, mashabiki wa bara hili wana mizuka ya hatari, ikiwa ni pamoja na kutumia rangi kujichora bendera ya utaifa wao.

9)Wachezaji wanaocheza Uingereza
Ligi kuu uingereza ina idadi kubwa ya mashabiki, kitu kinachopelekea mashabiki wote hivi sasa, kuelekeza macho yao huko. Marcos Rojo, Di Maria na Sergio Aguero wanafanya idadi ya mashabiki wa jiji la Manchester kuyafuatilia mashindano haya kwa ukaribu.

10)Mechi ya ufunguzi
Kawaida mechi za ufunguzi zinakua na msisimko wa hali ya juu. Chile wenyeji wakianza kwa ushindi mnono wa goli 2-0 dhidi ya Ecuador haikua mechi rahisi. Utamu wa mechi za ufunguzi unaleta radha ya kuyafuatilia mashindano hayo kongwe

0 comments:
Post a Comment