'Mlinda mlango huyo raia wa Jamhuri ya Czech ameripotiwa kuwa mbioni kujiunga na wiki hii lakini amekanusha vikali kuwa bado hajakubali kusaini mkataba na Arsenal.'
Kutokana na taarifa mbalimbali zilizoenea kuwa dili la Petr Cech kujiunga na Arsenal kukamilika, mlinda mlango huyo wa Chelsea ameamua kuandika moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii na kukanusha vikali taarifa hiyo.
Kuna uwezekano mkubwa sana kwa Cech kuhitimisha miaka yake 11 aliyoitumikia klabu hiyo yenye maskani yake Stamford Bridge na kuelekea kwa mahasimu wao wa jiji la London klabu ya Arsenal, kutokana na ufinyu wa nafasi yake katika kikosi cha kwanza baada ya ujio wa Mbelegiji Thibaut Courtois.
Hata hivyo ripoti zilionesha kuwa uhamisho wake ulikuwa ni kama tayari vile kujiunga na Arsenal, lakini Cech aliamua kuandika ujumbe kwenye akaunti yake ya twitter ambao pia alishirikiana na kampuni yake ya usimamizi inayojulikana kwa jina la- The Sports PR Company.
Ujumbe huo unasomeka hivi: "...kama tulivyowaeleza hapo awali, hakuna uhamisho wowote unaomhusu @PetrCech ambao umekamilika mpaka sasa -lolote litakalotokea kuanzia sasa@PetrCech atalitolea uthibitisho."
Mapema jana, John Terry alisema kuwa Arsenal watakuwa na faida kubwa endapo watafanikiwa kuinasa saini ya mlinda mlango huyo ambaye ni mzoefu na mwenye uwezo mkubwa, ambaye akiwa na Chelsea amefanikiwa kushinda mataji manne ya ligi kuu na FA na moja la klabu bingwa mwaka 2012.
0 comments:
Post a Comment